Biashara nyingi zinakufa kwa kushindwa kutoa bidhaa/huduma katika kiwango kinachotarajiwa na mteja (customer's expectation).
Katika mipango ya biashara (business plans), mabenki na taasisi zingine zitoazo fedha huweka mazingatio na msisitizo katika kipengele hiki, hii ni kwa sababu; kipengele hiki ndicho hushikilia uhai wa biashara yoyote ile.
Mteja huangalia ubora wa bidhaa/huduma katika mtazamo wa aina mbili
- Hali ya ushikiki (tangibility), hapa mteja huzingatia; uhakika wa bidhaa (reliability), dhana ya uzuri (aesthetics) na namna ambavyo bidhaa/huduma itatatua haja zake (serviceability)
- Hali isiyo ya ushikiki (intangibility), hapa mteja huzingatia; ufanisi katika utoaji wa huduma (customer care competency), upatikanaji wa bidhaa/huduma(access) na utulivu wa mazingira ya biashara.
- Kuhakikisha anafanya vifungashio (packaging), ikiwa bidhaa inaruhusu hali hiyo.
- Kuhakikisha anachagua eneo moja (focusing) katika mitazamo ya ubora tuliyoiangalia hapo juu mfano; suala la upatikanaji (access), hapa unahakikisha bidhaa/huduma inapatikana sokoni kwa wakati muafaka pia kwa kiwango muafaka. Uhudumu wa bidhaa/huduma (serviceability), hapa unahakikisha kwa mfano kama lengo la bidhaa yako ni kutibu matatizo ya ngozi kwa mtumiaji, basi hakikisha hili linatokea.
- Kutumia teknolojia katika biashara yako, hii itakusaidia kuepuka makosa ya kibinadamu ambayo hupelekea kuathiri ubora wa bidhaa/huduma husika. Mfano kwa mfanyabiashara kuanzia ngazi ya kati anapaswa kutumia program maalum za kompyuta katika mahesabu, usimamizi wa rasilimali watu n.k. Pia matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ni muhimu ili kuleta ukaribu na wateja.
- Matumizi ya malighafi (raw materials) yenye ubora unaostahili katika utayarishaji wa bidhaa.
0 comments